Pata Kupumzika Kidogo

Pata Kupumzika Kidogo

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. —MATHAYO 11:28

Katika 1 Wafalme 19, Nabii Eliya anaogopeshwa na vitisho vya Yezebezeli na anavunjika moyo sana hadi anataka kufa. Ni kitu gani ulimwenguni kilichomfanya Eliya, ambaye siku iliyokuwa imetangulia alikuwa amewashinda manabii 450 wa Baali, akajiruhusu ghafla kushikwa na hofu na kukata tamaa namna hiyo? Ukisoma kisa hicho vizuri, ni wazi kwamba alikuwa amechoka kabisa kwa kujisukuma sana kwa muda mrefu. Mwili na nia ya Eliya ilikuwa imechoka kabisa, na hisia zake zilikuwa zimesambaratika. Alikuwa mwoga, mwenye kufadhaika, mwenye kukata tamaa na akakosa tumaini.

Hakuna kitu ulimwenguni kinachoonekana kizuri kwetu kama tumechoka. Huwa inaonekana kwetu kwamba hakuna anayetupenda, hakuna anayetusaidia, na hakuna anayetujali. Huwa tunahisi kwamba hakuna anayetuelewa, tunatumiwa vibaya na kuteswa. Mara nyingi tunapohisi kwamba tuna matatizo ya ndani, tatizo letu kubwa huwa ni kwamba tumechoka.

Bwana alijua kwamba Eliya alikuwa amechoka. Kwa hivyo akampa utulivu wa mzuri wa usiku na sahani kadhaa za chakula. Lilikuwa jibu rahisi hivyo kwa tatizo gumu. Pengine jibu lako ni kama hilohilo. Pata utulivu mzuri unaohitajika, na ule lishe nzuri. Huenda vikawa vitu vya kiroho kabisa ambavyo utafanya leo!


Nguvu, hekima na ujasiri huja kutoka mahali pa utulivu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon