Roho ya Mshindi

Roho ya Mshindi

Lakini katika mambo hayo yote tunashinda na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. WARUMI 8:37

Unaishi maisha ya ushindi ndani ya Yesu? Iwapo la, huenda leo ndiyo siku yako ya kuanza kujiona kwa njia tofauti kuliko vile umekuwa awali, kujiona kama mtu ambaye hushinda hali ngumu, na sio kama mtu ambaye husita kwa hofu au kuhisi kulemewa kila wakati majaribu yanapokuja.

Unaona, huwezi kukwepa hali ngumu ni mojawapo ya sehemu za maisha, na huchukua mshindi kuzishinda. Yesu mwenyewe alisema kwamba tutakumbana na dhiki katika ulimwengu huu (tazama John 16:33). Paulo alielewa kuwa vikwazo haviwezi kuepukwa na akaandika katika Warumi 8:37 kwamba “tu washindi zaidi ya washindi” na kwamba “tutapata ushindi unaopita ushindi.”

Kuwa zaidi ya mshindi ina maana kwamba kabla ya kukabiliana na hali ngumu, kabla vita dhidi yako hata vianze, tayari unajua utashinda bora tu unamwamini Mungu na hukati tamaa. Hiyo ni ahadi ya kutufanya tushukuru—wewe ni zaidi ya mshindi ndani ya Yesu Kristo!


Sala ya Shukrani

Baba, nikiwa katika hali ambayo inanitisha au kuniogopesha, nitasimama kwenye Neno lako ambalo linasema mimi ni zaidi ya mshindi ndani yako. Asante kwamba sitashindwa kwa sababu uko nami, na unanilinda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon