Salama Ndani ya Yesu

Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. —YOHANA 15:5

Mungu anataka tumtegemee kikamilifu na kumtumainia kama vile tawi linavyoutegemea mzabibu. Tutakuwa tunakosa busara tukiweka tumaini letu katika mwili—ndani yetu au ndani ya mtu mwingine.

Umeweka tumaini lako ndani ya nguvu zako mara ngapi na ukashindwa vibaya? Ni mara ngapi watu wengine walienda kinyume na matarajio yako baada ya kuweka tumaini lako ndani yao? Ni mara ngapi umepata kusikitika watu wengine walipokukataa au kukosa kufanya ulichotarajia? Mungu ataruhusu tusikitishwe kila mara hadi tujifunze kumtegemea na kuweka tumaini letu ndani yake peke yake.

Sipendekezi kwamba tusiwe na tumaini lolote ndani ya watu, lakini tunafaa kutambua kwamba hawajakamilika na ni vigumu wao kukosa kutukosea. Yesu, hata hivyo, hatusikitishi! Yuko nasi kila wakati, na ni yeye pekee tunayeweza kuweka yake, matumaini yetu kamilifu.


Kuwa na mahusiano makuu na watu, lakini usitie matumaini ndani yao kuliko Mungu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon