Sema Machache; Onyesha Mengi

Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi msipokaa ndani yangu (YOHANA 15:4)

Kadri tunavyokuza uhusiano wetu na Mungu, ndivyo tunavyosisimka na kuwa na shauku zaidi na hivyo ni vyema. Hata hivyo, lazima tuwaonyeshe wat kitu zaidi ya msisimko; wanahitaji kuona ushahidi wa mabadiliko na tunda jema.

Paulo alisema kwamba, maisha yetu yanafaa kuwa barua ambazo watu wanaweza kusoma (2 Wakorintho 3:3). Kwa upande mwingine, tabia zetu huzungumza kwa sauti kuliko maneno au hisia. Kwa kipindi cha miaka mingi nimegundua kwamba, lazima msisimko na bidii vichanganywe na subira, wema, ukarimu, tabia nzuri, upole na hiari ya kusaidia watu. Kwa kweli matendo yetu huzungumza kwa sauti kuliko maneno. Bila shaka tunafaa kuwaambia watu kuhusu Yesu kwa sababu maneno yaliyozungumzwa kwa wakati unaofaa yanaweza kusaidia, lakini Wakristo wa kweli hujulikana kwa matunda yao.

Kadri unavyotumia muda zaidi kuwa na Mungu, ndivyo utakavyokuwa na matunda zaidi yanayotokana na uhusiano huo. Ni matunda mema yanayomtukuza Mungu na ni matunda mema yanayowazungumzia sana watu kwa sauti. Ninawajua watu niliojaribu kushawishi kwa maneno ambayo nilikuwa nimebadilisha na hawakuwahi kushawishika, lakini katika miaka iliyofuatia walihitaji usaidizi na nilipowasaidia, waligundua kwamba bila shaka Mungu alikuwa amefanya kazi ndani yangu. Ni vigumu sana kubishana na tunda jema, kwa sababu ni shahidi kwamba sisi ni wale tunaodai kuwa. Ninakuhimiza kuwa mwangalifu na jinsi unavyowatendea watu nyakati zote.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Kabla hii siku iishe, kuna uwezekano kwamba utakutana na watu wengi. Waache na tabasamu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon