Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu. MITHALI 2:6
Mungu hutaka tutumie hekima, na hekima huhimiza subira. Hekima husema, “Subiri kidogo tu hadi hisia zitulie, kabla ya kufanya au kusema kitu; halafu uchunguze uone kama ndicho kitu sawa kufanya.” Hekima huwa na shukrani kwa kile tayari unacho na kusonga kwa subira kwa kile alicho nacho Mungu tena kwa ajili yako.
Hisia hutusihi kuharakisha, zikituambia tunapaswa kufanya kitu na kukifanya saa hii! Lakini hekima ya kiungu hutuambia tusubiri hadi tutakapokuwa na picha dhahiri ya kile tunapaswa kufanya na wakati ule ambao tunapaswa kukifanya. Tunahitaji kuweza kuchukua hatua ya nyuma na kutoka katika hali zetu na kuziona kwa matazamo wa Mungu. Halafu tunaweza kufanya uamuzi kulingana na kile tunachojua badala ya kile tunachohisi.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru Baba, kwamba subira ni tunda la Roho ambalo ninaweza kuonyesha katika maisha yangu. Kwa usaidizi wako, ninadhamiria kufanya uamuzi leo kwa hekima na subira. Asante kwa kuniongoza njiani.