Takataka ya Wasiwasi

Takataka ya Wasiwasi

Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza, hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele. ZABURI 55:22

Wasiwasi ni haina maana kabisa. Vile nisemavyo kila mara, ni kama kubembea katika kiti cha bembea mchana wote—kinakushughulisha, lakini hakikufikishi popote. Tukianza kutazama wasiwasi kwa njia ya kiuhalisi tunaona ilivyo takataka. Nia zetu huzunguka karibu na shida bila kikomo, zikitafuta tu majibu yaliyo na Mungu peke yake. Kufikiri kuhusu kitu ndani ya neema ya Mungu huwa na amani, lakini wasiwasi hutesa.

Tunaweza kuomba na kumwambia atusaidie ili tusiwe na wasiwasi, lakini mwishowe lazima tuweke mawazo yetu kwa kitu kingine kuliko shida zetu. Kukataa kuwa na wasiwasi ni ushahidi kwamba tunamwamini Mungu—humwachilia kwenda kufanya kazi kwa niaba yetu. Iwapo unahiari kuacha kuwa na wasiwasi, basi utaweza kuingia katika nia ya kusherehekea na kutoa shukrani. Unaweza kumwamini Mungu na kufurahia maisha huku akisuluhisha shida zako. Jipe ruhusu ya kukoma kuwa na wasiwasi.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa kipaji cha amani. Nisaidie kukutafakari wewe badala ya kutafakari shida zangu. Ninakushukuru kwamba sihitaji kuachilia wasiwasi iyatawale maisha yangu; ninaweza kuchgua kuishi kwa imani kwa kukuamini.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon