Tambua Adui Yako

Tambua Adui Yako

Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka akitafuta mtu ammeze. 1 PETRO 5:8

Yohana 10:10 inasema “mwivi haji ila kuiba, kuua na kuharibu.” Mstari huo unamrejelea Shetani na mfumo wake. Vile tu Mungu alivyo na mfumo ambao anatuhimiza tuishi kulingana nao, na anaahidi baraka tukifanya hivyo, Shetani ana mfumo na anataka tuishi kulingana nao ili aibe baraka zetu.

Shetani hutuonyesha hali halafu anatuogopesha kuwa haitawahi kubadilika. Mungu anataka tuamini Neno lake ni la kweli hata kama bado tuko katikati ya hali hiyo. Ndiyo kwa sababu Andiko linasema, lakini katika mambo haya yote, tu zaidi ya washindi… (Warumi 8:37).

Katika uchumi wa Mungu, tunaweza kuamini kabla tuone mabadiliko au vitu vizuri tunavyotamani. Yesu alitupatia amani kama urithi wetu, lakini Shetani hufanya kila awezalo kutuibia amani hiyo. Tambua adui yako na usimame kwa bidii kinyume naye katika amani na nguvu za Mungu.


Sala ya Shukrani

Baba, ingawa nina adui anayejaribu kuniibia furaha yangu, asante kwamba sihitaji kumwogopa. Tayari umemshinda adui, na Roho wako anaishi ndani yangu. Ninatambua nina adui, lakini ninakushukuru kuwa tayari ushindi ni wangu kupitia kwa Kristo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon