Tarajia Kupokea

Tarajia Kupokea

Kwa ajili ya hayo, Bwana hungoja (kwa bidii akitarajia na kutafuta na kutamani) kuwa na huruma kwako; na kwa hivyo hujitukuza, ili akakurehemu na kukuonyesha ukarimu wake kwa upendo. Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa hukumu. Wamebarikiwa (kwa furaha, bahati, na ni wenye kuonewa kijicho ) wote wamngojao [kwa bidii] wanatarajia na kutafuta na kutamani (ushindi wake, kibali chake, upendo wake, amani yake, furaha yake, na urafiki wake usiovunjika wala kulinganishwa!] ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana Bwana ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao. —ISAYA 30:18

Ninataka uyashike haya kwa uthabiti katika moyo wako: Unaweza kufikiria kuhusu yale ambayo unafikiria! Matatizo ya watu wengi yanatokana na ruwaza za mawazo yao ambazo huzaa matatizo wanayokumbana nayo. Kumbuka kwamba matendo yako ni matokeo ya moja kwa moja ya mawazo yako. Na hata kama adui anampa kila mtu mawazo mabaya, huhitaji kukubali mawazo anayokupa.

Isaya 30:18 limekuja kuwa mojawapo ya maandiko ninayopenda. Ukilitafakari, litaanza kukuletea tumaini kuu…na uwezo mkuu. Katika andiko hili, Mungu anasema kwamba anatafuta mtu wa kuonea huruma (kumtendea mema), lakini hawezi kuwa mtu mwenye uchungu na mawazo hasi. Lazima awe mtu anayetarajia Mungu kuwa mwema kwake.

Kadri unavyobadilisha mawazo kwa wema, ndivyo maisha yako yatakavyobadilika kwa ajili ya wema wako. Utakapoanza kuona mpango wa Mungu juu yako katika mawazo yako, utaanza kutembea ndani yake.


Mawazo ndiyo kiongozi au mtangulizi wa mawazo na matendo yote. Unaweza kutarajia mambo mazuri kutoka kwa Mungu!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon