Timiza tu Sehemu Yako

Bwana ameisikia dua yangu; Bwana atayatakabali maombi yangu (ZABURI 6:9)

Kila mwaminio anaitwa kuzungumza na Mungu na kusikiza sauti yake kupitia kwa maombi, lakini sio kila mtu huitwa kwenye afisi ya kiroho ya uombezi. Kwa mfano, ninaamini Mungu amemwita Dave kama muombezi kwa ajili ya Marekani. Anaonekana kuwa na kazi “rasmi” kutoka kwa Bwana ya kuombea nchi yetu, mzigo wa kweli wa mambo na shughuli za kitaifa, hamu ya kutaka kuona uhuisho katika nchi yetu, na mvuto wa ndani wa kudumu wa vitu vinavyohusu Marekani. Husoma historia ya Marekani kwa bidii na kuwa na habari za kila wakati kuhusu kinachofanyika katika serikali ya nchi yetu. Kuna pia msukumo usio wa kawaida ambao huambatana na maombi yake. Hivyo ndivyo ninavyomaanisha kuhusu mtu anayefanya kazi katika afisi ya muombezi.

Tangu 1997, Nimekuwa nikimtazama Dave akiomba na kulia na kushambulia mbingu kwa niaba ya Marekani. Huwa silii kwa ajili ya nchi yetu vile anavyofanya yeye, lakini hilo halimaanishi kwamba sijali au kwamba siombei viongozi wetu. Inamaanisha tu kwamba siwezi kujilazimisha kuwa na uchu wa Dave kwa sababu alipewa uchu huo na Mungu. Inamaanisha pia kwamba Mungu ananitumia mimi na Dave kama timu; ana Dave akicheza katika nafasi moja na mimi nikicheza katika nyingine. Nikianza kufikiri nini kibaya nami kwa sababu sifanyi uombezi jinsi Dave anavyofanya, ninajileta chini ya hukumu- na hiyo itanizuia kutimiza kile ambacho Mungu ameniita kufanya. Lakini nikibaki nikiwa na uhakika katika nafasi yangu na kupania kufanya vizuri kabisa hapo, timu yetu itashinda kila wakati. Mungu hampi watu wote kazi zote. Roho Mtakatifu hugawia kila mtu kazi yake anavyoona yeye kwamba inafaa na tunachohotaji kufanya ni kutimiza sehemu yetu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Tulia na uombe jinsi Mungu anavyokuongoza.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon