Tulia Na Umjue Mungu

Tulia na Umjue Mungu

Acheni, mjue ya kuwa mimi ni Mungu, nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi! —ZABURI 46:10

Watu wengi leo hukimbia kutoka kwa kitu kimoja hadi kingine. Wana uraibu wa shughuli, na nilikuwa mmojawapo wa watu hao!

Kwa muda mrefu, nilihisi lazima nitafute kitu cha kufanya kila wakati. Ilikuwa lazima nihusike na kushughulika na kile kilichokuwa kikiendelea. Nikafikiri nisingeweza kukosa kitu chochote kwa sababu sikutaka kitu kifanyike bila mimi kujua. Nisingeweza kutulia. Ilikuwa lazima nifanye kitu. Sikuwa mwanadamu (human being) nilikuwa mwanadamu wa kufanya (human doing).

Ninashukuru, niligundua kuwa iwapo tutatulia, na tusijifanyie mambo, tutaona nguvu za ajabu za Mungu zikifanya kazi katika maisha yetu. Mara nyingi huwa tunafadhaishwa hadi mwisho kwa sababu tu tunajaribu kufanya vitu ambavyo Mungu peke yake anaweza kufanya. Mungu anataka kutuongoza, lakini ili kuhisi mwelekeo wake tunahitaji kuwa watulivu! Chukua muda kila siku kusikiliza. Tuna masikio mawili na mdomo mmoja, kwa hivyo Mungu alikusudia tusikilize zaidi kuliko kuzungumza.

Tunapokuwa na mipango na malengo, tunaweza kumpa Mungu (ili kumtambua), ili kuhakikisha kwamba tuna amani na pia mpango!


Mungu hutwaa kile kilicho cha juu na kizuri kwa wanaomwamini. Tulia na uache adhihirishe nguvu zake katika maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon