Tunda la Roho Mtakatifu

Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole (WAGALATIA 5:22-23)

Tunapojazwa kwa Roho Mtakatifu kiasi cha kububujika, tunaona tunda lake likidhihirika kupitia kwetu. Tuna amani na furaha na kuwa wazuri kwa watu. Yesu ametuamrisha kupendana jinsi alivyotupenda. Ni muhimu kwa ulimwengu kuona upendo huu ukidhihirishwa. Watu wa ulimwengu wana shauku ya ukweli na wanahitaji kuona kwamba Mungu anaweza kubadilisha watu. Wanahitaji kuona upendo wa Mungu katika matendo ili kuwafanya wawe na shauku na kiu yake.

Biblia inatufundisha kwamba, tunafaa kuwa mwanga na chumvi (soma Mathayo 5:13-14). Ulimwengu uko gizani, lakini Wakristo waliojazwa na Roho Mtakatifu huleta mwanga kila wanakoenda. Ulimwengu hauna ladha, lakini Wakristo huleta chumvi kwa maisha wanapokuwepo.

Tuna kazi kubwa ya kufanya kama Wakristo na tunafaa kuwa wahisivu kwa Roho Mtakatifu kila mara kuhusu vile tunavyowatendea watu. Mungu yuko ndani yetu akiusihi ulimwengu kupitia kwetu; sisi ni waakilishi wake binafsi (soma 2 Wakorintho 5:20). Kwa mtazamo wa ukweli huo, Paulo alisema tushikilie kibali cha kiungu tulichopewa. Lazima tufanye kazi na Roho Mtakatifu ili kukuza tunda la Roho Mtakatifu hadi ukamilisho ili tuwe wenye mwenendo unaomtukuza Mungu na kuvuta watu kwake.

Tunda la Roho hukuzwa tunapopitia mambo magumu maishani na kuendelea, kwa usaidizi wa Mungu kutendea watu mema jinsi yeye anavyowatendea. Kuwa na nguvu ndani ya Bwana na kumbuka kwamba ulimwengu unakutazama na unakuhitaji kuwa chumvi na mwanga.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Hata kama utakabiliana na changamoto gani leo, endelea kuwa mkarimu kwa kila mmoja unayekutana naye.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon