Uaminifu katika Ukame

Uaminifu katika Ukame

Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku, katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. —ZABURI 63:1

Hata hivyo, haijalishi tunavyompenda Bwana na haijalishi tunavyomkaribia, sisi wote hupitia katika nyakati za ukame… nyakati ambazo vitu vichache hutuhudumia, au kunyunyizia maji nafsi zetu. Tunaenda kanisani, lakini hatuhisi tofauti yoyote tunapotoka kuliko tulivyohisi tulivyofika pale. Tunapitia katika nyakati ambazo tunahisi kwamba maombi yetu ni makavu, na nyakati ambazo hatuwezi kusikia au kuhisi chochote kutoka kwa Mungu.

Nimepitia katika nyakati za kilele cha mlima, na nimepitia nyakati za bonde. Nimekuwa na nyakati kavu katika maisha yangu ya maombi na katika sifa na ibada zangu. Kumekuwa na nyakati ambazo ningeweza kumsikia Mungu kwa waziwazi, lakini kumekuwa na nyakati zingine ambazo sikusikia lolote kabisa.

Unapopitia msimu kama huu, usiache ukulemee. Mungu yuko nawe, hata kama unahisi uwepo wake au la. Mkristo mkomavu haachi uhusiano wake na Mungu uamuliwe na vile anavyohisi. Unaweza tu kuchagua kuamini kwamba Mungu yuko nawe leo. Unaweza kufanya uamuzi wa kumpenda na kumwabudu Mungu kwa imani. Unaweza kuomba, uamini anakusikia, na kuamini kwamba atakupa kila kitu unachohitaji. Ukifanya uteuzi huu, utapata amani mpya katika kutembea kwako na Bwana, na utakuwa thabiti katika kila msimu wa maisha yako.


Mungu anakupenda na yuko papa hapa nawe—uwe unahisi au huhisi. Kuwa mwaminifu katika ukame na katika kilele cha mlima pia.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon