Uko Huru Kutokana na Yaliyopita

Uko Huru Kutokana na Yaliyopita

Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hivyo simameni wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. WAGALATIA 5:1 BIBLIA

Watu wengi hubaki wakiwa wamenaswa katika yaliyo nyuma. Lakini kitu kimoja tu kinachoweza kufanywa kuhusu yaliyo nyuma, na hiyo ni kusahau. Shukuru kuwa ukimuomba, Mungu husamehe na kusahau yaliyo nyuma…na pia wewe waweza.

Tunapofanya makosa, vile sisi wote hufanya, tunaweza tu kuomba msamaha wa Mungu na kusonga mbele katika uhuru ambao Yesu alitupatia. Kama Paulo, sote tunachuchumilia mbele ili kufikia alama ya utimilifu, lakini hakuna aliyewasili.

Ninaamini sababu mojawapo ambayo ilifanya Paulo akafurahia maisha na huduma yake ni kwa sababu alikusudia kuyasahau yaliyo nyuma na kuyaweka nyuma (tazama Wafilipi 3:13–14). Kama sisi, alikuwa akichuchumilia mbele hadi kwenye alama ya utimilifu, akikubali alikuwa hajawasili, lakini alikuwa na ufahamu wa jinsi ya kufurahia maisha yake huku akiwa safarini.

Hebu tufuate mfano wa Paulo. Usikwame kwa yaliyo nyuma—ishi katika uhuru wa msamaha leo!


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba, yangu yaliyo nyuma nimeyaacha nyuma. Umenisamehe dhambi zangu na kunipa mwanzo mpya. Ninakubali msamaha wako na ninadhamiria kuishi maisha yangu ya sasa na ya siku zijazo kwa ajili ya utukufu wako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon