Ulinganifu wa Sauti Tamu

Ulinganifu wa Sauti Tamu

Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. WARUMI 14:19

Nilipokuwa nikihudumu katika kanisa, Mungu alinipa mfano mkubwa wa maana ya kuishi kwa ulinganifu na kila mmoja.

Niliiambia timu yote ya ibada kurudi kwenye jukwaa, kisha nikawaomba kuimba na kucheza wimbo waliochagua. Bila shaka nilijua wote watachagua wimbo tofauti kwa sababu sikuwa nimewaambia wimbo watakaoimba au kucheza.

Walipoendelea kuimba na kucheza, sauti ilikuwa mbaya ajabu! Hakukuwa na ulinganifu. Kisha nikawauliza kucheza “Yesu Ananipenda.” Ilisikika ikiwa tamu, yenye kutuliza, na kufariji kiajabu.
Kutokuwa na ulinganifu ni kelele kwa masikio ya Mungu. Lakini tukiishi katika ulinganifu, tunatoa sauti tamu. Tunapojifunza thamani ya kila mmoja, tunakuwa wenye shukrani kwa ajili ya kila mmoja na tunajifunza kufanya kazi pamoja.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa ajili ya watu ambao umetia katika maisha yangu. Ninataka kuishi kwa ulinganifu sio ugomvi, ili uhusiano wangu uwe sauti tamu kwa masikio yako. Asante kwa kunipa subira na hekima ya kuishi kwa ulinganifu na wengine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon