Umuhimu wa Kwanza

Umuhimu wa Kwanza

Uache mabaya ukatende mema, utafute amani ukaifuatie! —ZABURI 34:14

Kuwa na amani ni jambo linalofaa kupewa umuhimu wa kwanza katika maisha yetu. Katika Zaburi 34:14, Daudi anatuagiza kuifuatia amani, kuitamani na kuitafuta. Hivyo ndivyo amani ilivyo muhimu.

Masikitiko na mfadhaiko ni adui wa kawaida wa amani. Wakati mwingi, ili kukabiliana na hawa wanaoharibu amani, kuna haja kwetu kupanga tena mambo muhimu kwanza na kuachilia vitu ambavyo havizai matunda.

Ukitaka kuishi katika amani ya Bwana, fanya uamuzi wa kutopita mipaka yako. Huku vitu vingi katika maisha yako vikiwa muhimu, je, vyote ni vya haja kweli? Fikiria kuhusu hilo kidogo. Anza kuangalia maisha yako, waza kuhusu shughuli zisizozaa matunda matunda yoyote, na uanze kuzipuna. Wewe ndiwe ulipanga ratiba yako na ni wewe pekee unayeweza kuibadilisha.

Ni muhimu sana kuacha kujishughulisha kupita mipaka. Mwombe Mungu hekima na ufuate uongozi wake kuhusu kile utakachojihusisha nacho na mahali ambapo unafaa kutumia nguvu zako. Ukifanya hivyo, utatambua kwamba kutumia wakati naye litakuwa jambo la kwanza—mengine yote ni ya baadaye. Unapomfanya Mungu kuwa umuhimu wa kwanza, na ukitafuta mwelekeo wake kuhusu jinsi ya kutumia muda na nguvu zako, baada ya hapo utashangazwa na amani itakayokuja katika maisha yako.


Unaweza kutulia katika hakikisho kwamba Mungu yuko nawe kwa yote unayokabiliana nayo. Hakupi tu amani— ni amani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon