Umuhimu wa Uombezi

Umuhimu wa Uombezi

Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi… — EZEKIELI 22:30

Kufanya uombezi kunamaanisha kusimama katika pengo kwa niaba ya mtu, kumtetea mbele za Mungu. Kukiwa na kuvunjika kwa uhusiano kati watu na Mungu kwa sababu yoyote ile, tuna faida ya kujiingiza katika pengo lililotokea na kuwaombea. Tunaweza kuwaombea na tutarajie kuwaona wakiwa wamefarijika na kuhimizika huku wakingoja. Tunaweza pia kutarajia wakati wa upenyo wa kutimizwa kwa hitaji lao kuja watakapokuwa wanalihitaji zaidi.

Sijui ningefanya nini kama iwapo watu wasingeniombea. Huwa namwomba Mungu kunipa watu watakaoniombea na kwa kutimilizika kwa huduma aliyoniitia. Tunahitaji maombi ya uombezi ya kila mtu.

Maombi kwa wengine ni sawa na kupanda mbegu. Lazima tupande mbegu ndipo tuvune mavuno (Wagalatia 6:7). Kupanda mbegu katika maisha ya watu wengine kupitia kwa uombezi ni njia moja inayotuhakikishia kuvuna mavuno katika maisha yetu. Kila wakati tunapomwombea mtu mwingine, tunamwalika Mungu sio tu kufanya kazi katika maisha ya mtu huyo lakini pia yetu.

Uombezi ni njia mojawapo muhimu sana ya kuendesha huduma ya Yesu Kristo ambayo alianzisha hapa ulimwenguni.


Tunaweza kuachilia nguvu za Mungu katika maisha ya watu wengine kwa kuwaombea.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon