Unapohisi Kufadhaika

Unapohisi Kufadhaika

Na amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. —WAFILIPI 4:7

Miaka mingi iliyopita, nilienda kwa daktari kwa sababu nilikuwa nikiugua kila mara. Aliniambia dalili zilikuwa matokeo ya mfadhaiko. Sikuwa ninapata usingizi wa kutosha, na nilikuwa nikila kwa njia isiyofaa, na kujisukumiza kwa nguvu.

Mfadhaiko ni sehemu ya kawaida ya maisha ya kila mtu. Mungu ametuumba kustahimili kiasi fulani cha shinikizo na fadhaa. Tatizo hutokea tunaposukuma zaidi kuliko tunavyoweza kustahimili na kupuuza onyo ambayo mwili hutupatia unapodhurika au unapochoka.

Ninawahimiza kujitunza vizuri, kwa sababu ukitumia vibaya mwili ulio nao, huwezi kwenda dukani kununua mpya. Vitu vingi tunavyofanya ambavyo hutupatia mzigo mkubwa wa mfadhaiko ni vitu ambavyo tunaweza kubadilisha tukitaka. Jieleze ukweli kuhusu kwa nini unafanya baadhi ya mambo unayofanya na uache Mungu akusaidie kupogoa yanayokuchosha, na bila kuzaa matunda.

Amani inatakiwa kuwa hali ya kawaida kwa kila aaminiye katika Yesu Kristo. Yeye ni Mfalme wa Amani, na ndani ya Yesu, tunapata urithi wetu wa amani. Ni zawadi kutoka kwa Roho Mtakatifu, ambayo huwa anatupatia tunapoishi kwa kutii Neno lake.


Amani ambayo Yesu anatoa hutenda kazi katika nyakati nzuri na mbaya. Amani yake hutenda kazi katikati ya dhoruba.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon