Unaweza Kuwa na Hakika

Unaweza Kuwa na Hakika

Maana mioyo yetu yetu itamfurahia, kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu. ZABURI 33:21

Mungu anataka tuishi na hakika na kukabili maisha kwa ujasiri—na tunaweza kushukuru kwamba anasaidia kufanya yote mawili. Fanya uamuzi leo wa kuanza kuondoa shaka zaidi. Huenda ikawa hatua ya ujasiri kwako kama umeishi muda mrefu wa maisha yako katika hofu na kuwa na shaka, lakini ni muhimu ikiwa unataka kufurahia maisha yenye amani. Kuwa na shaka si mahali palipo na amani.

Weka tumaini lako ndani ya Kristo na vile wewe ulivyo ndani yake, sio katika vile watu wanafikiria juu yako. Jijue! Jua moyo wako, na usingoje watu wengine kukuamrishia ukweli kuhusu thamani yako. Usichukulie kwamba una makosa wakati wote mtu anapokosa kukubaliana nawe. Amini kwamba hekima ya Mungu inaishi ndani yako. Amini kwamba unaweza kufanya uamuzi. Hakuna haja ya kuamini kitu hasi kujihusu wakati ambao ni rahisi kuamini kitu chanya kujihusu—na bila shaka ina faida zaidi.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba tumaini langu haliko ndani yangu mwenyewe au ninayoyaweza; tumaini langu liko ndani ya Kristo Yesu. Ninaamini kwamba nina hekima na utambuzi wako. Leo nitaishi maisha ya ujasiri na tumaini.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon