ungu ni Mwema…kila Wakati

Mungu ni Mwema…kila Wakati

. . . Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu. LUKA 18:19

Mungu ni mwema. Wema ni mojawapo ya sifa za kitabia za Mungu tunafaa kushukuru kwayo. Na kwa kuwa wema ni sehemu mojawapo ya tabia zake, tunaweza kutarajia kuwa atatuitika kwa wema wakati wote. Mungu sio mwema tu wakati fulani; ni mwema kila wakati. Ni mwema kwa watu wasiostahili. Hutusaidia hata kama tumefanya vitu vibaya, iwapo tutakubali tu makosa yetu na kuomba usaidizi wake kwa ujasiri.

Tunaweza kuomba usaidizi wa Mungu wakati wote: “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.” ( Yakobo 1:5).

Habari njema ilioje! Mungu atatupatia amani tukiwa na majaribu—atafanya mlango wa kutokea. Shukuru kwamba, kile tunachohitaji kufanya ni kuomba, na atatupatia bila kututafutia makosa. Ajabu!


Sala ya Shukrani

Baba, nikiwa katika hali ambapo ninahitaji hekima yako na upaji wako, ninaomba kwamba utanipa kile ninachohitaji haswa. Ninakushukuru kwamba wema sio tu kitu unachodhihirisha, ni utu wako haswa. Ninakupenda na kukushukuru kwa wema wako leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon