Upande wa Ufufuo wa Msalaba

Upande wa Ufufuo wa Msalaba

Ili nimjue yeye na uweza wa kufufuka kwake, ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake. WAFILIPI 3:10 BIBLIA

Tunaweza kujifunza kuishi katika upande wa ufufuo wa msalaba. Yesu hakusulubiwa tu; tunashukuru kwamba alifufuliwa kutoka kwa wafu pia ili tusikwame katika dhambi, tukiendelea kuishi maisha ya chini, yenye ufukara na dhiki.

Mara nyingi kanisani tunaona msalaba wenye sanamu ya Yesu. Ninajua sanamu hizo hukusudiwa kumkumbuka na kumtukuza, hilo halina tatizo. Lakini, ukweli ni kwamba hayuko msalabani tena. Ameketi katika falme za mbinguni na Baba yake, na anafurahia kuishi maisha ya ufufuo.

Tunaweza kusherehekea kwa furaha kwamba Yesu alikuja kutuinua kutoka kwa ukawaida, kutoka kwa fikra hasi, hatia, aibu, na hukumu. Alikuja kupeleka dhambi zetu msalabani na kuzishinda. Hazina nguvu juu yetu tena kwa kuwa tumesamehewa—adhabu ya dhambi imelipwa. Tunaweza kuishi katika upande wa ufufuo wa msalaba na tukae katika falme za mbingu naye kupitia kwa imani.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kuwa na nguvu za ufufuo wa Yesu katika maisha yangu. Asante kwa kuwa Yesu alishinda dhambi na mauti, na kwa sababu Roho wako anaishi ndani yangu, ninaweza kuishi maisha ya ushindi na kushinda kila wakati.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon