Uponyaji Kwa Hisia Zilizoharibika

Uponyaji Kwa Hisia Zilizoharibika

Roho ya Bwana Mungu i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. —Isaya 61:1

Uponyaji wa hisia ni mada muhimu, kwa sababu maisha yetu ya ndani ni muhimu kuliko maisha ya nje. Warumi 14:17 inatujulisha kwamba ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, (si vitu vya nje), bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu (vitu vya ndani). Pia Luka 17:21 ufalme wa Mungu umo ndani yetu.

Kwa sababu ya dhuluma nilizopitia nikiwa mtoto, nilikuwa “mfungwa wa hisia” kwa muda mrefu. Lakini Mungu ameniponya na kunibadilisha na upendo wake. Na atakufanyia alivyonifanyia!

Katika Isaya 61:1, Bwana alisema kwamba amekuja kuponya waliovunjika mioyo. Ninaamini hilo linamaanisha wale waliovunjika ndani, waliopondwapondwa na kuumizwa ndani. Yesu anataka kukuongoza kutoka kwa uharibifu wa kihisia hadi mahali pa afya, uzima, na ukaribu na Mungu. Mkaribishe katika kila eneo la moyo wako na uache kazi ya uponyaji ianze!


Mungu atakutana nawe popote utakapokuwa na kukusaidia kufika unakohitaji kuwa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon