Urekebishaji wa Nia ya Kiungu

Na mfanywe wapya katika roho ya nia zetu. —WAEFESO 4:23

Mungu hutaka tudumishe nia nzuri ya roho kwa sababu mbili. Kwanza, humtukuza na kuhimiza watu wengine kudumisha nia nzuri ya roho wanapokuwa na matatizo; na pili, inamruhusu kufanya kazi katika maisha yetu, kutuletea usaidizi na ukombozi kutokana na kung’ang’ana kwetu.

Kuwa na nia nzuri ya roho kila wakati ni kitu kigumu hadi tupokee neema ya Mungu kutuwezesha kufanya hivyo. Yesu alisema pasipo yeye hatuwezi lolote (Yohana 15:5), lakini kupitia kwake tunayaweza mambo yote (Wafilipi 4:13). Usingoje hadi ujaribiwe kisha uwe na nia mbaya ya roho, lakini omba kila siku kwamba hata kitu gani kifanyike, unaweza kukivumilia huku ukiendelea kudumisha nia nzuri ya roho. Tutakuwa tukijaribiwa wakati wote, lakini tunaweza kuomba ili tusianguke katika majaribu.

Nia nzuri ya roho ni mojawapo ya rasilmali zetu kuu. Hutufanya tuwe wenye tumaini kamilifu bila kujali kinachofanyika katika maisha yetu.


Muombe Mungu ajaze nia yako ya roho kwa Roho Mtakatifu kila wakati!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon