Ushindi Juu Ya Vita

Ushindi Juu ya Vita

. . . Basi sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani ya andiko. —Warumi 7:6

Kuna nyakati katika maisha tunapolazimika kukabiliana na mfadhaiko, lakini tunaweza kuwa juu yake, sio chini yake. Kupitia kwa uongozi na nguvu za Roho Mtakatifu, tunaweza kushughulikia kazi zetu kwa urahisi badala ya mfadhaiko. Tunapoendelea kufuata uchochezi wa Roho, tutajua jinsi ya kushughulikia kila hali tunayokabiliana nayo.

Sisi sote tuna hali tusizopenda ambazo hutujia. Lakini kwa nguvu za Mungu, kupitia hizo hali huku tukijiepusha na mfadhaiko pia. Kadri tunavyoegemea, na kumwamini Mungu, ndivyo maisha yanavyokuwa mepesi. Kila hali maishani sio “rahisi,” lakini tunaweza kuzishughulikia kwa kile ninachokiita “Wepesi wa Roho Mtakatifu.” Kwa maneno mengine, Mungu hututia nguvu kufanya chochote tunachohitaji kufanya kupitia kwake. Hututia nguvu na kutusaidia.

Mungu atatuongoza, lakini tunahitaji kumwamini vya kutosha ili kufuata maelekezo yake. Huwa hatupatii ushauri wowote ambao si wa faida na kuendelea kwetu katika maisha. Mungu anakuelekeza mahali pa ushindi na shangwe, sio mahali pa kushindwa. Unapoendelea kufuata mwongozo wake, ninaamini utapitia mfadhaiko mchache kuliko wa siku zote. Huenda akakuchochea usifanye kitu unachotaka kufanya, au kufanya kitu usichotaka kufanya, lakini utiifu kwa uongozi wake hutuzuia kuchukua njia mbaya katika maisha na kupoteza muda na nishati!


Kutii tu uchochezi wa Roho Mtakatifu kutatuliza mfadhaiko haraka sana.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon