Ushuhuda Huja Baada ya Mtihani

Ushuhuda Huja Baada ya Mtihani

…Mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta subira. Yakobo 1:3

Mimi hupenda kusikia ushuhuda mkubwa wakati wote, lakini ninajua pia kwamba nyuma ya maelezo yasiyo ya kawaida ya maisha ya mtu, huwa kuna aina fulani ya changamoto au matatizo. Tunaweza kupita aina zote za mitihani tunapopitia maisha haya, na kuipita mitihani hiyo ni sehemu mojawapo ya kukataa kukata tamaa. Ni muhimu kwetu kuelewa nafasi muhimu ya majaribu na mitihani katika maisha yetu, kwa sababu kuelewa hutusaidia kuvumilia na kushukuru kwa athari za kutiwa nguvu ambazo mitihani na majaribu hayo hutupatia.

Kila kitu ambacho Mungu huturuhusu kupitia, bila shaka mwishowe kitakuwa kizuri kwetu—hata kama ni kigumu. Tunapokumbana na majaribu na mitihani, tukiikumbatia, tutajifunza mafunzo yatakayotusaidia katika siku zijazo.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie nipate kuwa na amani yako katikati ya mtihani ambao huenda ninaukabili. Ninakushukuru kwamba kila kitu unachoniruhusu kupitia kitafanya kazi kwa mema yangu. Na ninakushukuru kuwa unanipa nguvu ninayohitaji ili kushinda.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon