Usifadhaike Kuhusu Mustakabali

Usifadhaike Kuhusu Mustakabali

Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. MATHAYO 6:34

Fadhaa, hofu na woga ni “wezi maarufu wa amani.” Vyote ni uharibifu kabisa wa nguvu; havizalishi matokeo yoyote mazuri. Na tunaweza kupinga kila moja kwa nguvu za Roho Mtakatifu.

Mungu ametuandaa kukabiliana na maisha jinsi yanavyokuja, lakini tukiishi leo tukiwa na wasiwasi kuhusu kesho, tutajipata tukiwa tumechoka na kufadhaika. Mungu hatatusaidia kufadhaika. Kila siku huja na ya kutosha kwetu sisi kufikiri kuyahusu; hatahitaji kufikiria kuhusu hali za kesho huku tukiwa tunajaribu kuishi leo.

Suluhu tu ya pekee ya wasiwasi ni kujisalimisha kabisa kwa Mungu na mpango wake. Hata wakati vitu visivyopendeza vinapofanyika, tunaweza kushukuru Mungu kwamba ana uwezo wa kuvifanya vigeuke kwa mema yetu tukiendelea kuomba na kumwamini (tazama Warumi 8:28).


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwa kuwa ninaweza kuchagua kutokuwa na wasiwasi. Licha ya hali zangu, ninaweza kukutazama wewe na kuamini mpango wako juu ya maisha yangu. Asante kwamba unafanya kazi pamoja na vitu vyote kwa mema yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon