Unirudishie furaha ya wokovu wako; unitegemeze kwa roho ya wepesi. ZABURI 51:12
Mustakabali wako hauna nafasi katika nyuma yako, na ninakuhimiza usikwame katika wakati au kipindi cha wakati katika maisha yako ambacho kilipita. Mamilioni ya watu hukosa leo kwa sababu pengine wanakataa kuachilia yaliyopita au wana wasiwasi kuhusu mustakabali. Vitu maishani kama vile dhuluma na uchungu—vitu ambavyo vilifanyika kwangu na wengineo mamilioni—kusema ukweli ni vya kusikitisha. Dhuluma kama hizo hutia kiwewe na hutuathiri, lakini tunaweza kupata nafuu.
Mungu ni Mkombozi na Mhuishi—hicho ni kitu cha kushukuru kwacho kila siku. Anaahidi kuhuisha nafsi zetu. Kuna tumaini zuri katika kujua kwamba tukimwalika ndani na kushirikiana na mchakato wake wa uponyaji, Mungu atatuhuisha na kutupatia maisha ya nyakati za kiungu naye zilizojaa furaha.
Sala ya Shukrani
Baba, ninakushukuru kwamba sihitaji kuishi nikiwa nimekwama kwenye mambo ya nyuma. Wewe ni Mkombozi na Mhuishi, na unataka kuleta uponyaji katika maisha yangu. Asante kwa kuwa ya nyuma yangu yamekwisha na nina mustakabali mzuri wa kutazamia.