Usimsahau Mungu

Kwa maana watu wangu huwa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji (YEREMIA 2:13)

Kosa la kwanza na kubwa ambalo mtu yeyote anaweza kufanya ni kumuacha au kumpuuza Mungu, au kutenda kama ambaye hayupo. Hivi ndivyo ambavyo watu ambao Yeremia aliandika kuhusu katika andiko la leo walifanya. Baadaye katika sura hiyo hiyo iliyo na andiko hilo, Mungu anasema, “Watu wangu wamenisahau mimi kwa muda siku zisizo na hesabu” (Yeremia 2:32). Mkasa ulioje; inasikika ni kama Mungu amehuzunika au hata ni mpweke.

Kwa hakika sitapendezwa watoto wangu wakinisahau. Siku nyingi haziishi kabla sijazungumza na kila mmoja wao. Nina mwanangu wa kiume mmoja anayesafiri sana kwa sababu ya huduma. Hata akiwa ng’ambo huwa ananipigia simu kila baada ya siku chache.

Ninakumbuka wakati ambao mimi na Dave tulishiriki chajio na mmojawapo wa watoto wetu mara mbili mtawalia. Ilhali siku iliyofuatia alipiga simu kutaka kujua tulichokuwa tukifanya na kuuliza iwapo tulikuwa tunataka kufanya kitu pamoja jioni iliyofuatia. Alipiga pia akasema yeye na mkewe wanashukuru kwa mambo yote tunayofanya ili kuwasaidia.

Hizi ndizo aina za vitu vinavyosaidia kujenga na kudumisha mahusiano mazuri. Wakati mwingine, hivyo vitu vidogo vina maana kubwa. Matendo ya watoto wangu hunifanya nijue kwamba wananipenda. Hata ingawa ninajua kwa nia yangu kwamba wananipenda kwa hakika ni vizuri pia kuhisi upendo wao.

Hivyo ndivyo Mungu alivyo nasi, watoto wake wapendwa. Huenda akajua kuwa tunampenda, lakini anataka pia kuhisi upendo wetu kupitia kwa matendo yetu, hususan kumkumbuka na kutamani kwetu kutumia muda wetu naye.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu anajali kila kitu kinachokuhusu, kwa hivyo kuwa huru kuzungumza naye kuhusu kitu chochote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon