Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali amtumainiye Bwana atakuwa salama. Mithali 29:25
Hatutawahi kutimiza makusudi yetu kama tutajali kuhusu kile watu wanafikiria. Acha wafikiri wanachotaka. Kile mtu anafikiria juu yetu hakihitaji kutuathiri kabisa kwa sababu ukweli ni kwamba fikra zao haziwezi kutudhuru tusipokuwa na wasiwasi kuzihusu. Kitu ambacho kinafaa kuwa muhimu kwetu ni kile Mungu anafikiria kutuhusu. Sio sifa yetu mbele ya watu iliyo muhimu, lakini ni sifa yetu mbinguni iliyo muhimu.
Usijali kuhusu vile watu wengine wanafikiria, kwa sababu haitabadilisha wanachofikiria hata hivyo. Shukuru kwamba Mungu anakupenda na kuwa na fikra za juu kukuhusu—hilo ndilo muhimu! Iwapo utakuwa huru kuhusu kujali sana vile watu wengine wanavyofikiri juu yako, utapandisha kiwango chako cha maisha mara moja. Utaongeza furaha yako na amani yako kwa asilimia moja.
Sala ya Shukrani
Baba, kwa usaidizi wako, nitaacha kuwa na wasiwasi kuhusu kile watu wengine wanafikiria kunihusu. Ninakushukuru kwamba unanipenda na unaniwazia mema. Nisaidie kutambua kwamba hilo ndilo muhimu.