Usipigane, Omba tu

Usipigane, Omba tu

Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi. 2 MAMBO YA NYAKATI 20:17

Wakati mwingi Mungu hutuambia kufanya kitu au kutupatia kazi na tunaanza kufanya. Lakini adui huja kinyume nasi, na tunapogeuka kupigana naye, tunageuka kutoka kwa Mungu. Ghafla adui anapata umakinifu wetu. Tunatumia muda wetu tukipigana dhidi yake badala ya kuomba na kumwambia Mungu kuingililia kati.

Ninataka ujue hiki: adui siye hasa shida yako; ni shida ya Mungu. Utaharibu wakati ukiondoa umakinifu wako kutoka kwa kazi na nafasi ulizopewa na Mungu na kuanza kummakinikia shetani.

Shetani anajua kwamba anaweza kukuhangaisha, mwishowe akushinde. Mungu ni mtetezi wako; anaahidi kupigana vita vyako. Kwa hivyo adui akianza kuchochea dhoruba katika maisha yako, shukuru kwamba Mungu ana ushindi na ufanye hivi vitu rahisi: omba na umuamini Mungu.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa nguvu za maombi. Badala ya kujaribu kupigana vita vyangu mwenyewe, ninakupa wewe leo. Ninashukuru kwamba, adui anapokuja kama mafuriko, mimi ni zaidi ya mshindi kupitia kwako (tazama Warumi 8:37).

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon