Vita vya Upendo

Vita vya Upendo

Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana, kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. 1 PETRO 4:8

Mojawapo ya vitu vya ajabu ambavyo nimejifunza na ambacho bado kinausisimua moyo wangu ni kwamba upendo ni vita vya kiroho. Huu ukweli hufanya vita vya kiroho visisimue, kwa sababu kupenda watu hufurahisha.

Petro wa kwanza 4:8 inatufundisha kuwa na upendo mwingi kwa kila mmoja. Tafsiri ya King James inatumia neno bidii kumaanisha “kushika moto, au kuchemka.” Safari yetu ya upendo inahitaji kushika moto na kuchemka, sio kuwa baridi na kukosa kudhihirika.
Upendo wetu ukishika moto, Shetani hatatuweza. Huenda tukasema “hakuna anayetuweza.” Ushawahi kupika kitu kwenye wimbi-mikro kwa muda mrefu ukashindwa kukiondoa kwa sababu kilishika moto sana? Tunafaa kutamani kuwa hivyo.

Shika moto wa upendo—moto wa kupindukia kiasi kwamba shetani hawezi kuugusa!


Sala ya Shukrani

Ninashukuru, Baba, kwamba unanipenda. Nisaidie kufuata mfano wako na kuwapenda watu walio karibu nami. Asante kwamba bila kujali vile watu wanavyonitendea, bado ninaweza kuwapenda kwa upendo wako mtimilifu usio na masharti.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon