Vitu vya Kwanza, Kwanza

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. —MATHAYO 6:33

Mara nyingi huwa tunatumia muda wetu wote kwa kutafuta mali, baraka, majibu ya shida zetu, wakati ambao kile tunatakikana kufanya ni kutafuta tu Mungu. Kadri tunavyomtafuta Mungu kwa sababu tu tunataka kuwa katika uhusiano naye, ndivyo kila kitu katika maisha yetu kinalainika.

Awali katika miaka yangu ya huduma, nilimtafuta Mungu kuhusu vile ningefanya huduma ikue. Matokeo ni kwamba ilibaki vilevile. Haikukua haraka kama nilivyotarajia, na wakati mwingine hata ilirudi nyuma. Nilichokosa kutambua wakati huo ni kwamba kile nilihitaji kufanya kilikuwa kutafuta ufalme wa Mungu, na angeongeza ukuaji.

Ukweli ni kwamba hatuna lazima ya kumsihi Mungu kutupatia chochote. Iwapo anachotaka ni mapenzi yake, atatupatia kilicho chema kwa wakati mzuri. Tunachohitaji kufanya ni kumpenda Mungu na kumtafuta kwanza na tutake kufanya vitu anavyotaka tufanye. Tunapofanya hivyo, tutaanza kumkaribia Mungu ambapo ni muhimu ili tuweze kukabili mafanikio kwa njia nzuri, au baraka za vitu za Mungu.

Tafuta uwepo wa Mungu kila wakati, na sio zawadi za Mungu. Atakupa vitu vingi vizuri, lakini anahitaji nafasi ya kwanza katika maisha yetu. Hatufai kuwa na miungu mingine kabla yake!


Tafuta Mungu kabla ya kitu chochote, kaa ndani yake, na utamkaribia kuliko wakati mwingine wowote.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon