Wakati Muhimu Sana wa Siku

Ee Mungu, Mungu wangu, nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku, katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji. — ZABURI 63:1

Mungu hupendezwa ukitumia muda kuwa naye katika ushirika na ibada kila siku. Ni wakati huu wa kuwa na Mungu ambao utabadilisha jinsi unavyoona maisha, kukupa nguvu unayohitaji ili kushinda, na kukuleta karibu zaidi na Mungu.

Mara nyingi ni katika nyakati zetu za siri na Mungu ambapo huwa anafanya kazi ndani kabisa katika mioyo yetu. Ni wakati wa ndani unaotumia kuwa na Mungu, ukimpenda tu na kumruhusu kukupenda, ambao utakufanya ukue na kuona mabadiliko ya kweli ya kiroho yakifanyika.

Kuna shughuli nyingi katika maisha na kutakuwa na visababu kila mara vya kutotumia muda kuwa na Mungu. Kazi za kufanya zitakuwepo wakati wote, kupiga simu, kufanya usafi, na kadhalika. Lakini ukidhamiria kumweka Mungu kwanza, kumtafuta bila kujali vizuizi vya siku, utatuzwa pakubwa.

Kadri unayotumia muda wako kuwa na Mungu, ndivyo unavyokuwa na hakika, amani, furaha, nguvu, kibali na ushindi zaidi. Yeye ndiye chanzo cha hivi vitu vyote. Ukijitolea kutumia muda wako naye, vitatiririka katika maisha yako kama kawaida.


Hakuna kitu muhimu katika maisha yako kuliko uhusiano wako wa kibinafsi na Yesu kristo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon