Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali, mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yetu huleta subira. Subira na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. —YAKOBO 1:2–4
Mara nyingi huwa hatuoni inapofanyika, lakini Mungu anashughulika na mpango wake mtimilifu juu ya maisha yetu kisiri. Ingawa tunataka matokeo saa hii, kujenga tabia nzuri huchukua muda na subira.
Biblia inasema kwamba subira hufanya kazi timilifu katika maisha yetu. Tunapomngoja Mungu, anatujenga kabisa na kikamilifu, bila kupungukiwa na chochote. Nimegundua kwamba subira ni zaidi ya uwezo wa kungoja; ni uwezo wa kuwa na moyo mtulivu unapongoja. Hili tunda tekelezi la Roho hutokana na uhusiano wa karibu na Mungu—hujidhihirisha kwa moyo mtulivu wenye matumaini bila kujali hali.
“Wakati wa Mungu mara nyingi huwa si kama wetu. Wakati wote tuko mbioni lakini hayuko mbioni. Yeye huchukua muda kufanya mambo kwa njia sawa—Huweka msingi imara kabla ajaribu kujenga jengo. Sisi ni mjengo wa Mungu unaondelea kujengwa. Yeye ni Mjenzi Mkuu, na anafahamu anachofanya.
Unapohisi kwamba huna subira, kumbuka kwamba wakati wa Mungu wakati wote huwa mtimilifu!