Watu Wote Wanaweza Kumsaidia Mtu

Watu Wote Wanaweza Kumsaidia Mtu

Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote. 1 WATHESALONIKE 5:15

Kutamani kitu hakuzalishi matokeo tunayotaka. Chochote ambacho Mungu anakuongoza kufanya, fuatilia kwa bidii kile kinachohitajiwa kufanywa ili ufanikiwe kupata matokeo hayo.

Wakati mmoja nilisikia kisa kuhusu watu wanne walioitwa Watu wote, Mtu fulani, Mtu yeyote na Hakuna mtu. Kulikuwa na kazi muhimu iliyohitaji kufanywa, na Watu wote walikuwa na hakika kwamba Mtu fulani angeifanya. Mtu yeyote angeifanya, lakini Hakuna mtu aliyeifanya. Mtu fulani alikasirika kuhusu hilo kwa sababu ilikuwa kazi ya Watu wote. Watu wote walifikiri Mtu yeyote angeifanya, lakini Hakuna mtu aliyetambua kwamba Watu wote wasingeifanya. Mwishowe Watu wote walimlaumu Mtu fulani wakati ambao Hakuna mtu aliyefanya kile ambacho Mtu yeyote angefanya.

Funzo la kisa hiki ni rahisi: Unapoona kwamba kitu kinahitaji kufanywa na una uwezo wa kukifanya, kuwa mwenye shukrani kwa nafasi ambayo Mungu amekupa basi nenda ukawe mabadiliko ambayo kila mmoja anasubiria.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwa nguvu na hivi vipaji ambavyo umenipa. Nionyeshe unachotaka nifanye, na unisaidie kukifuatilia kwa moyo wangu wote. Kwa usaidizi wako, ninajua ninaweza kuleta tofauti.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon