Weka Moyo wako Huru

Weka Moyo wako Huru

Utusamehe deni zetu kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. —MATHAYO 6:12

Yesu alizungumza kuhusu haja kusamehe wengine mara kwa mara.

Iwapo tutaishi katika uhusiano wa karibu na Mungu, ni muhimu kuwa wepesi wa kusamehe. Kadri tunavyosamehe haraka ndivyo inakuwa rahisi kuishi kwa amani. Inaturuhusu kukabiliana na shida hiyo kabla ikite mizizi katika hisia zetu. Uchungu utakuwa mgumu zaidi kung’oa iwapo una mizizi mirefu yenye nguvu.

Tunapomshikia mtu kifundo, hatumdhuru huyo mtu—tunajidhuru wenyewe. Kukosa kuwasamehe watu wengine hakuwabadilishi, lakini hutubadilisha. Hutufanya tuwe na kisirani, uchungu, dhiki na wagumu wa watu kuwa karibu nasi. Fikiria hivi, unapofikiria umeshikilia kifundo, ni kifundo haswa kinachokushikilia.

Kutokusamehe ni njia danganyifu ya shetani ya kutuweka katika utumwa. Anataka tufikiri tunalipiza kisasi, kwamba tunajilinda kutokana na kudhuriwa tena, lakini hakuna mojawapo la ukweli. Kutokusamehe kunaendelea kukudhuru na kukuzuia kumkaribia Mungu.

Mtu akikudhuru, ninakuhimiza kumwomba Mungu neema ili kumsamehe huyo mtu ambaye umemshikia kifundo. Amua kuanzia hapa na kuendelea kuuweka moyo na maisha yako huru kutokana na hisia hasi haribifu.


Inawezekana tu kuwa na afya nzuri kihisia ukiachilia uchungu wote na kutokusamehe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon