Yaone mambo madogo

Yaone mambo madogo

Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya. 1 Wathesalonike 5:11

Siku moja nilipoingia katika jengo la ofisi, mtu mmoja aliyekuwa karibu akanifungulia mlango wangu. Nilimshukuru na kutabasamu.

Alisema, “Wewe ndio mtu wa tano nimefungulia mlango,” na wewe ni wa kwanza kutabasamu na wa pili kunishukuru. “Nilimshukuru mara ya pili, huku nikitabasamu sana . Baadaye, nilifikiria kiasi gani tunachochukua wengine kama si kitu, hata katika mambo rahisi, kama kufungua mlango kwa mgeni.

Mara nyingi tunathamini watu wanapokuwa wanafanya mambo makuu kwetu, lakini ni mara ngapi tunafurahia mambo madogo? Mtu anapofanya kitu kizuri kwako na unamshukuru, huwajenga na kuwahamasisha. Ina maana sana kwao, kama ilivyokuwa kwa mtu huyo katika jengo la ofisi.

Je! Basi lako liliwasili kwa wakati? Ikiwa ndivyo, umemshukuru dereva? Wakati wa mwisho ulikula kwenye mkahawa, je ulimshukuru msaidizi kwa kujaza kikombe chako cha kahawa kwa mara ya pili bila kuulizwa? Hili ni jambo ambalo nataka ufanye: endeleza mtazamo wa shukrani kwa watu katika maisha yako.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nisaidie ili nione mambo madogo, ambayo watu wananifanyia. Sitaki kukosa kuwa na shukrani. Badala yake, nataka kuwashukuru na kuwajenga.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon