Yesu akawakazia macho, akawaambia, kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana. —MATHAYO MTAKATIFU 19:26
Watu wengi ninaokutana nao hutaka kuanzia hatua ya A katika maisha yao ya Kikristo, wakonyeze macho yao mara mbili, na wajikute katika hatua ya Z. Wengi wao husikitika kwa kutokujua vipawa vyao ama kile Mungu amewaita kufanya katika maisha yao. Wengine wanaogopa sana kutofaulu na kufanya makosa kiasi cha kuwazuia kujaribu.
Sisi wote tuna uwezo ambao haujatumiwa, lakini hatutawahi kuuona ukitokea hadi tutakapoamini kwamba tunaweza kufanya lolote ambalo Mungu amesema tunaweza kufanya katika Neno lake. Hadi tuchukue hatua ya imani, huku tukiamini kuwa kwa Mungu hakuna lisilowezekana, hawezi kufanya kazi anayotaka kufanya ndani yetu ili kujenga uwezo wetu. Huchukua kushiriki na kupenda kwetu kupitia kwa imani, uamuzi wetu, utiifu na bidii ya kazi kujenga alichoweka ndani yetu.
Hakuna anayeweza kutuamulia, lakini tunaweza kujiamulia. Ikiwa hatujaamua, shetani ataiba kila kitu tulicho nacho. Ninakuhimiza kuuchipuza uwezo wako kwa kuufanya kitu kinachoonekana. Hutawahi kujua unachoweza kufanya ikiwa huwa haujaribu kufanya kitu chochote. Usiogope kuanza kufanya kitu ambacho unaamini Mungu anakuongoza kufanya. Utakapochukua hatua, utagundua kuwa una uwezo wa kufanya mambo makuu.
Kuwa jasiri, kuwa mkakamavu, na uwe yote unayoweza kuwa!