Amani Inayokuja na Kuridhika

Amani Inayokuja na Kuridhika

Ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. 1 Timotheo 6:8

Hakuna mtu aliye na maisha matimilifu, na kuna uwezekano kwamba unapotaka maisha ya mtu mwingine, pia yeye anataka ya mwingine; labda hata anataka maisha yako.

Watu wasiojulikana wanataka kuwa wahusika wakuu katika sinema, wahusika wakuu wa sinema wanataka usiri. Mwajiriwa wa kawaida anataka kuwa mwajiri, lakini mwajiri anatamani asingekuwa na wajibu mwingi kama alio nao. Mwanamke ambaye hajaolewa anataka kuolewa, lakini mara nyingi mwanamke aliyeolewa anatamani asingekuwa na mume.

Kuridhika maishani sio hisia—ni uamuzi. Kuridhika hakumaanishi kuwa hatutaki kuona mabadiliko au ubora, lakini inamaanisha kwamba tunashukuru kwa kile Mungu ametupatia na tunadhamiria kufurahia kipaji cha maisha.


Sala ya Shukrani

Ninapojaribiwa kuhusudu maisha mtu mwingine, Baba, ninaomba kuwa unisaidie kuridhika na vile nilivyo na kile ulichonipa. Ninakushukuru kwamba nina kusudi kwa ajili ya maisha yangu. Ninachagua kushukuru na kuridhika leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon