Mungu ana Vitu Vizuri kwa ajili Yako

Mungu ana Vitu Vizuri kwa ajili Yako

Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? WARUMI 8:32

Watu wengine huonekana kuwa na wazo kwamba ili kuwa Mkristo lazima uache kila kitu kinachokufurahisha lakini sio ukweli. Mungu ni upendo, ni mwema, na yeye hutaka tufurahie vitu vizuri. Biblia inasema Mungu hutupa vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha (tazama 1 Timotheo 6:17). Mungu anatupenda sana, alimtuma Mwanawe Yesu kuchukua dhambi zetu na kutupa uzima, na uzima tele tele (tazama Yohana 3:16; 10:10). Hicho ni kitu cha kushukuru kwacho daima! Kitu chochote ambacho Mungu hutufundisha tusifanye ni kwa ajili ya faida yetu. Tunatii amri zake kwa wema wetu kulingana na Neno la Mungu.

Tunapompokea Yesu, tunapokea ufalme wa Mungu ndani yetu, na ufalme huo ni haki, amani, na furaha ndani ya Roho (tazama Warumi 14:17). Tunaweza kuchagua kuendelea kuishi na dhiki, masikitiko, mfadhaiko, huzuni, wasiwasi, hatia, kuhumika na hofu, lakini Yesu anataka tupokee uhuru kutokana na vitu hivyo. Mungu hataki tuvibebe kila tunakoenda. Kupitia kwa Yesu, tunaweza kuishi maisha yenye furaha tele, ya kushinda na ya wingi vile tulivyokusudiwa kuishi.


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kutambua kwamba huna kingine ila vitu vizuri kwa ajili ya maisha yangu. Asante kwamba hata unaponisahihisha na kunifundisha, unanionyesha njia bora ya kuishi. Ninashukuru kwa wema wako na maisha yenye furaha ninayoweza kuwa nayo ndani yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon