Bila Uchungu, Hakuna Faida

Bila Uchungu, Hakuna Faida

. . .Roho ya Bwana Mungu i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. —ISAYA 61:1–3

Tunapoendelea kupata ukamilifu wa kihisia, hata chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, uchungu wa uponyaji kutoka kwa vidonda vya kihisia unaweza kuzidisha kiwewe kuliko uchungu tunaopitia wa mwili. Kwa sababu nilipitia uchungu mwingi wa kihisia mapema katika maisha yangu, nilichoka kudhurika. Nilikuwa ninajaribu kupata uponyaji kwa kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu, ilhali sikuelewa kwa nini utaratibu huo ulikuwa wa uchungu mwingi.

Bwana akanifunulia kwamba nimekuwa nikijificha nyuma ya “milango wazi ya uchungu.” Nilikuwa katika utumwa mbaya, nikijificha katika nafsi za danganyifu, kujifanya na unafiki. Nilianza kuelewa kwamba watu wanapoondolewa katika utumwa hadi kwenye uhuru, lazima wapitie tena katika milango wazi ya uchungu ili kufika upande ule mwingine wa milango hiyo. Hupitia majibu ya hisia za uchungu wao wa awali huku Bwana akiwaongoza kukabiliana na masuala, watu, na ukweli ambao ni mgumu. Habari njema ni kwamba, hatulazimiki kukabiliana nayo peke yetu. Yuko karibu nawe kila mara, na atakuleta mahali pa uponyaji ukimruhusu.


Shukuru Mungu, anaponya waliovunjika mioyo, kufungua milango ya jela, na kuweka huru mateka! Huna lazima ya kuishi katika uchungu wa mambo yaliyopita!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon