
Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; maana njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu asiye na uovu, yeye ndiye mwenye haki na adili. —KUMBUKUMBU LA TORATI 32:4
Mungu hutupenda bila masharti. Hatupendi tukiwa wazuri halafu kuacha kutupenda tunapokuwa wabaya. Hutupenda kila wakati. Ni mwenye huruma wakati wote, asiyekasirika haraka, mwingi wa neema na mwenye rehema, tayari kutoa kila wakati.
Mungu ni Mwamba, usiobadilika na bila mkengeuko. Ni mkuu, asiyeshindwa, mwaminifu na mwenye haki, mkamilifu na kuwa sahihi katika yote afanyayo. Hatawahi kutuacha wala kutusahau.
Ni kitu gani kitakachofanyika katika maisha yetu na maisha ya wale walio karibu iwapo tungekuwa zaidi kama Mungu? Ni kitu gani kingefanyika iwapo tungekuwa tunaonyesha upendo kila wakati, tusio na hasira za haraka, wenye kujawa neema pamoja na rehema, tayari kusamehe kila wakati? Ni kitu gani kingefanyika iwapo kama alivyo Mungu wetu, tungekuwa wenye fikra chanya, amani, na ukarimu? Yeye ni Mwamba wetu, lakini ni mfano wetu pia. Tunafaa kung’ang’ana kuwa vile alivyo.
Sisi sote tunaweza kukua kiroho na kubadilishwa katika mfano wa Kristo. Mungu hatutarajii kuwa wakamilifu mara moja, lakini anataka kutusaidia kuwa kama zaidi na zaidi kama yeye siku baada ya nyingine.
Mungu hutusaidia kuwa zaidi na zaidi kama yeye. Usikate tamaa kwa safari ndefu uliyo nayo—furahia kwamba unakua!