Acha mto uendelee kupita

Acha mto uendelee kupita

Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Yohana 7:38

Kama waumini katika Kristo, Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu, anakaa katika roho zetu. Yeye ni mto wa uzima ndani yetu. Mto huu ni zawadi nzuri sana iliyotolewa kwa kila mmoja wetu na Mungu. Unapita na afya nzuri, mtazamo mzuri juu ya maisha, na mtazamo wa ukarimu na wa kusamehe.

Watu wengi, hata hivyo, wameruhusu mto wao kusimamishwa. Wao daima hukata tamaa, na haijalishi wanafanya nini, hawawezi kuonekana kuacha. Miaka ya kupuuza imegeuza mto uliokuwa wenye nguvu katika mkondo mdogo. Unajua watu kama hawa? Je! Hii inaonekana kama maisha yako?

Hadi pale utakapoweza kupata mto wako uondolewe taka na kufunguliwa, kila kitu kitakuwa kigumu, kukatisha tamaa na kutokuwa na furaha. Hutaweza kuonja maji ambayo yanatuliza kuliko kitu kingine chochote.

Fanya uchaguzi leo kuacha kutumia muda wako kwa mapigano yako ya maisha, ukujitahidi na kutembea katika matope kwa kila hatua. Mwombe Mungu akusaidie kuondoa uchafu. Atakuonyesha kinachozuia mtiririko na jinsi ya kuiondoa. Kisha, furahia mtiririko wa kuridhisha wa mto wa uzima!

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, nataka kuweka Mto wako wa maji yaliyo hai upite ndani yangu. Nionyeshe uchafu huo unaozuia njia na kisha unionyeshe jinsi ya kuuondoa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon