Dhabihu ya Sifa

Dhabihu ya Sifa

Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. —WAEBRANIA 13:15

Sifa ni nafasi ya kukaa, kushukuru, na kuhesabu wema wa Mungu katika maisha yetu. Na sifa ni kitu ambacho unaweza kufanya bila kukoma. Tunaweza kumsifu kwa kazi zake kuu, maajabu aliyoumba, na hata kazi za neema ambazo atafanya katika maisha yetu bado. Tunaweza pia kumsifu kwa upaji wake wa kila siku.

Dhabihu ya sifa inamaanisha kuitoa hata kama hatujihisi kuitoa. Kama waaminio, katika nyakati ngumu na pia nzuri, tunaweza kumsifu Mungu kwa wema, rehema, huruma wenye upendo, neema, na uvumilivu. Huku tukingoja kuona utimizaji wa maombi, tunaweza kuchagua kukubali na kukiri na kutukuza jina lake.

Sio wajibu wetu kuwa na wasiwasi na kuhangaika au kujaribu kufanya sehemu ya Mungu kwa kuchukua mikononi mwetu hali ambazo zinafaa kuachiwa yeye peke yake. Badala yake ni wajibu wetu kumtwika tu Bwana mizigo yetu (1Petro 5:7), huku tukimwamini na kusifu kwa yale aliyotenda, anayotenda, na yale tunayoamini kwa imani kwamba anaenda kufanya. Hata katika siku ambazo si rahisi—wakati ambao hatuoni vile mambo yote yatakavyofanya kazi—tunaweza kutoa dhabihu ya sifa. Hili humpendeza Bwana na kuzidisha imani yetu tunapomtumainia bila kujali hali zinazotuzunguka.


Naomba dhabihu ya sifa iwe vinywani mwetu bila kikomo kwa kazi ajabu za neema ambazo ametutendea.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon