Epuka Ulinganishi

Epuka Ulinganishi

. . . Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao hawana akili… —2 WAKORINTHO10:12

Iwapo umekabiliana na shaka ya usalama katika maisha yako, ufunguo muhimu wa kushinda shaka hiyo ni: Usiwahi kujilinganisha na mtu yeyote kwa sababu ni kukaribisha hisia za kujiona duni.

Ninataka kukuhimiza kukoma kujilinganisha na watu wengine kuhusu vile unavyofanana, cheo ulicho nacho, au muda unaotumia kuomba. Ulinganishi hufanya ujifikirie ulivyo na kutatiza mpango wa Mungu juu ya maisha yako.

Hivyo hivyo tutakuwa na busara tukijiepusha na kulinganisha majaribu yetu na yale ya watu wengine. Unaweza kuwa unapitia mambo magumu, lakini usimwangalie mtu mwingine na kusema, “Kwa nini haya yanafanyika kwangu ilhali kwako yalikuwa mepesi?”

Yesu alimfunulia Petro kabla ya muda, baadhi ya mateso ambayo angepitia. Mara tu Petro akataka kulinganisha mateso na matatizo yake katika maisha na ya mtu mwingine kwa kusema, “Na huyu mtu je?” Yesu akajibu kwa kusema, “Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe nifuate Mimi!” (Yohana 21:22).

Hilo jibu ni lake kwetu sisi pia. Hatujaitwa kujilinganisha, ila kukubaliana na mapenzi yake juu yetu.


Mungu anataka ujue kwamba wewe ni wa kipekee na ana mpango wako binafsi maalum kwa ajili ya maisha yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon