Fanya Uwe wa Kibinafsi

Ninyi mmekuwa rafiki zangu mkitenda niwaamuruyo (YOHANA 15:14)

Katika andiko la leo, Yesu anatuambia sisi ni marafiki zake tukimtii. Katika andiko linalofuatia, anasema hatuiti vijakazi wake tena ila marafiki zake. Ni wazi kwamba, anataka uhusiano nasi mwenyewe na anataka tuwe sisi wenyewe naye. Anathibitisha hili kwa ukweli kwamba anaishi ndani yetu. Ni kiasi gani kingine zaidi ambacho mtu mwenyewe anaweza kuingia ndani ya mtu kuliko kuishi ndani ya mtu mwingine?

Iwapo Mungu angetaka uhusiano wa mbali, wa kibiashara, au uhusiano wa kitaalamu nasi, angeishi mbali sana nasi. Huenda angekuwa akitembea mara mojamoja, lakini bila shaka asingekuja kuwa na makao ya kudumu katika nyumba moja nasi.

Yesu alipokufa msalabani, alifungua njia kwetu ya uhusiano wa kibinafsi na Mwenyezi Mungu. Wazo lilioje hilo! Hebu tu fikiria: Mungu ni rafiki yetu wa kibinafsi!

Tunapomjua mtu mashuhuri, huwa tunasema, “Aha, mtu huyo ni rafiki yangu. Mimi huenda kwake kila mara. Huwa tunatembeleana kila wakati.” Tunaweza kusema hivyo hivyo kuhusu Mungu tukiwa na ushirika naye, kusikiliza sauti yake na kutii anachosema, na kukaa katika uwepo wake kila siku.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unaweza kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Mungu; ni rafiki yako.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon