Fikra za Imani

Fikra za Imani

Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza. —MWANZO 39:21

Hata ingawa Yusufu alikuwa anaadhibiwa bila makosa kwa sababu alifungwa kwa kitu ambacho hakufanya, Bwana alikuwa naye bado, akimpa kibali cha kimiujiza na kumtunza. Alithibitisha kwamba mtu huwa hajaharibika sana hata kama ataishia kwenda jela iwapo Mungu atampa kibali.

Hata kitu gani kifanyike maishani mwetu, tunaweza kuwa na kibali kwa Mungu hata watu (Luka 2:52). Lakini kama vitu vingine vizuri katika maisha, ati kwa sababu tu vitu vipo, haimaanishi kwamba tutakuwa navyo. Mungu huwa anaachilia vitu vingi kwetu ambavyo huwa hatuvipokei na kuvifurahia kwa sababu hatujawahi kuchochea imani yetu.

Kwa mfano, tukienda kwenye mahojiano ya kazi huku tukikiri hofu na kushindwa, tutahakikishiwa kutopata kazi hiyo. Kwa upande ule mwingine, hata kama tutatuma maombi ya kazi ambayo tunajua hatujahitimu kikamilifu kuifanya, tunaweza kwenda kwa tumaini, tukiamini kwamba Mungu atatupatia kibali katika kila hali ambayo ni mapenzi yake.

Mungu hataki tuwe na woga wa matatizo tunayokabiliana nayo katika maisha. Yuko usukani, na atafanya mambo yote kuwa mema kwa ajili yetu tukimpenda na kumwamini.


Yusufu alidumisha fikra nzuri katika hali mbaya. Alikuwa na “fikra za imani,” na Mungu akampa kibali.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon