Fuata hekima ya Mungu, sio hisia zako mwenyewe

Fuata hekima ya Mungu, sio hisia zako mwenyewe

Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu; Mithali 2:6

Maisha hayana furaha wakati tunaruhusu hisia zetu zitawale. Hisia zinabadilika siku baada ya siku, saa baada ya saa, hata wakati kwa wakati. Mara nyingi hutudanganya. Kwa kifupi, hatuwezi kuamini hisia zetu. Lakini tunaweza kuchagua, kama wafuasi wa Kristo, kupuuza hisia za uwongo na kuishi kwa kweli na hekima. Hebu niwape mifano fulani … Labda umejikuta katika umati wa watu na ukahisi kama kila mtu anazungumzia juu yako. Hiyo haina maana wao walikuwa wanazungumza juu yako. Labda unahisi kwamba hakuna mtu anayekuelewa, lakini hiyo haimaanishi hawakuelewi. Unaweza kujisikia kutoeleweka, usiyethaminiwa au hata uliyenyanyaswa, lakini hiyo haimaanishi wewe uko hivyo. Hizi ni hisia tu. Tunahitaji kuwa watu wazima, wenye tahadhari, walioamua kutembea katika Roho. Inachukua hatua ya mara kwa mara ya hiari kuchagua mambo ya njia ya Mungu badala ya njia yetu. Hata ingawa tunaweza kujisikia mara kwa mara tukiwa na hisia mbaya, hatuwezi kuruhusu hisia hizo kudhibiti na kuharibu maisha yetu. Badala yake, tunaweza kuchagua kufuata ukweli-hekima ya Mungu, ujuzi na ufahamu.

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, hisia zangu mara nyingi zinapingana na hekima yako na kujaribu kunidanganya, lakini siwezi kuziruhusu kuendesha maisha yangu. Nipelekeze kwa ukweli wako ili nipate kukaa na uhusiano na Wewe na nisibalishwe na hisia zangu za kubadilika kila mara

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon