kupokea nguvu za Mungu kupitia sala

kupokea nguvu za Mungu kupitia sala (

Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; Waebrania 5:7

Sala ina nguvu kwa sababu inaunganisha mioyo ya watu duniani na moyo wa Mungu mbinguni. Tunapoomba, tunaungana na Mungu, naye huathiri maisha yetu ya kila siku zaidi ya ufahamu wetu. Ninaamini sala ni mojawapo ya mamlaka kuu zaidi katika ulimwengu wote. Hiyo inaweza kuonekana kama tamko la ujasiri, lakini ni kweli!

Sala hufungua mlango wa Mungu kufanya kazi. Ni shughuli ambayo wewe na mimi tunaweza kushiriki duniani wakati tunahitaji nguvu ya mbinguni kuja katika maisha yetu na kuleta hekima, mwongozo, himizo au mafanikio ya ajabu.

Sala inatuunganisha kwa nguvu za Mungu-na kwa hiyo ni nguvu kubwa kuliko kitu kingine chochote tunaweza kufikiria. Hata Yesu alihitaji kuomba na kupokea nguvu hii wakati alipokuwa duniani.

Nguvu ya Mungu inaweza kuleta amani na furaha, kutoa hekima, kutoa hisia ya thamani na kusudi la maisha ya mtu, na kufanya kila aina ya muujiza. Je! Unataka kuona kazi ya nguvu katika maisha yako? Basi fanya sala kuwa kipaumbele.

OMBI LA KUANZA SIKU

Bwana, nguvu ya sala ni ya kushangaza kabisa. Ninataka kuunganishwa na Wewe na kukuona ukifanya kazi katika maisha yangu, kwa hiyo nitajitolea sasa kubaki katika hali ya sala ya mara kwa mara na Wewe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon