Fupi na Rahisi

Fupi na Rahisi

Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. —MATHAYO 6:7– 8

Ninaamini iwapo ninaweza kurahisisha maombi yangu na kukosa kuleta utata katika suala ninaloombea kwa kutumia maneno mengi, maombi yangu yatakuwa dhahiri na yenye nguvu.

Tunaweza kuchagua kutumia nguvu zetu kuachilia imani yetu, sio kurudiarudia vifungu na kurefusha tu maombi. Ninakumbuka wakati mmoja nilipata ikiwa vigumu kufupisha na kurahisisha maombi yangu. Nikaanza kutambua kwamba tatizo langu katika kuomba lilikuwa kwamba sikuwa na imani kuwa maombi yangu yangeleta majibu yakiwa mafupi, rahisi na yalenge lengo. Nilikuwa nimeingia katika mtego wa kiakili ambao watu wengi huingia—“urefu—ni—bora” Sitetei kuwa tuombe tu kwa muda mfupi peke yake, lakini ninapendekeza kwamba kila maombi yawe rahisi, ya moja kwa moja, yalenge lengo, na yajae imani.

Sasa ninapofuata mwelekeo wa Mungu wa kuyarahisisha na kuomba bila kujirudiarudia, ninaona nikiachilia imani kuu. Na huwa ninajua kwamba Mungu amesikia na atajibu.


Iwapo maombi yako yana utata, yarahisishe. Kumbuka, unasikika kwa sababu ya imani yako, sio kiasi chako cha maneno!

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon