Furaha ni Uamuzi

Furaha ni Uamuzi

Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, tutashangilia na kuifurahia. ZABURI 118:24

Kufurahia uzima tele ambao Yesu alikufa ili kukupa hutegemea uamuzi unaofanya, sio hali zako. Shukuru kuwa unaweza kuamua kufurahi ukiwa mahali hapo ulipo na kufurahia maisha uliyo nayo sasa hivi ukiwa njiani kuelekea unakoenda. Unaweza kufanya uamuzi thabiti kufurahia safari yako.

Unaweza kuanza kwa kusema kwa sauti kuwa, “Nitafurahia maisha yangu.” Hadi hilo wazo liimarike katika nia yako, kila asubuhi unapoamka, kabla uondoke kitandani, ninakuhimiza kutangaza kwa sauti kwamba, “Nitafurahia siku hii! Ninakamata siku! Ninachukua mamlaka dhidi ya shetani—mwizi wa furaha—hata kabla hajajaribu kuja kinyume nami. Nimeamua kwamba nitakuwa na furaha leo!” Kuwa na nia sawa ya mawazo husaidia katika kila hali.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba ninaweza kuchagua kuishi katika uzima tele ambao Yesu alikufa kunipa. Sihitaji kuishi maisha ya dhiki, yasiyo na furaha. Ninaweza kuchagua kusherehekea wema wako na kufurahia maisha uliyonipa.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon